Methamphetamine

From Wikipedia, the free encyclopedia

Methamphetamine
Remove ads

Methamphetamine [note 1] ni kichocheo cha mfumo mkuu wa neva (CNS) ambacho hutumika hasa kama dawa ya kulevya na mara chache sana katika kutibu ugonjwa wa upungufu wa tahadhari, Nakolepsia (ugonjwa wa usingizi wa ghafla) na unene uliokithiri.[12] Matumizi yake kwa unene uliokithiri hayapendekezwi tena. Inapochukuliwa kwa mdomo, athari zake huanza ndani ya dakika 30 na zinaweza kudumu hadi masaa 24.[13][9]

Ukweli wa haraka Jina la (IUPAC), Data ya kikliniki ...

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na shinikizo la juu la damu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kuinua hali ya mhemko, matatizo ya kulala, kutetemeka, kuhara na matatizo ya ngono. Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha hisia zisizo za kweli (psychosis), hali ya msisimko wa kupindukia (mania), kifafa, joto la juu la mwili, na mishtuko ya misuli isiyo ya hiari (tics).[13] Kuna hatari kubwa ya unyanyasaji; ingawa vifo vinavyohisiana moja kwa moja na matumizi yake ni nadra.[13] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto na kunyonyesha baada ya kuitumia hakupendekezwi.[13] Dawa hii ni katika familia ya ya madawa ya amfetamini.[13]

Methamphetamine iligunduliwa mwaka wa 1893 na ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1919. Mara nyingi hutengenezwa katika vituo visivyo halali nchini Marekani na Mashariki ya Mbali.[9] Kwa burudani, inaweza kumezwa, kukoromwa, kudungwa au kuvutwa kama sigara.[9] Imeainishwa kama dutu inayodhibitiwa na Ratiba II.[9] Uzalishaji, usambazaji na umiliki wa methamphetamine umezuiwa au umepigwa marufuku katika nchi nyingi. Katika Ulaya. iligharimu takriban Euro 17 hadi 64 kwa gramu kwa usambazaji haramu kufikia mwaka wa 2018. Takriban watu milioni 27 walitumia amfetamini, nyingi zaidi ya methamphetamine, mwaka wa 2019.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads