Michelle Obama

Mwanasheria na Mke wa raisi mstaafu wa Marekani. From Wikipedia, the free encyclopedia

Michelle Obama
Remove ads
Remove ads

Michelle LaVaughn Obama (jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson; alizaliwa 17 Januari 1964) ni Mwanasheria wa Marekani na ndiye mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama.[1] Huyu ndiye wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwa mke wa Rais wa Marekani.

Thumb
Michelle Obama.

Michelle alizaliwa na kukua katika kitongoji cha South Side ya Chicago na kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu katika Kitivo cha Sheria cha Harvard.

Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu akaja kuwa mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.

Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini Washington, D.C.


Remove ads

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka


Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads