Muhammad Ali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa watu wengine wenye jina hili tazama Muhammad Ali (maana)
Muhammad Ali | |
Takwimu | |
---|---|
Jina | Muhammad Ali |
Jina la kuzaliwa | Cassius Marcellus Clay Jr. |
Jina la utani | The Greatest, The Champ, The Louisville Lip |
Urefu | 1.91 m (6 ft 3 in) |
Kufikia | 2 M |
Aina ya michezo | Mchezo wa ngumi |
Mgawanyiko wa uzito | Uzito mkubwa |
Utaifa | Marekani |
Tarehe ya kuzaliwa | 17 Januari 1942 |
Mahala pa kuzaliwa | Louisville, Kentucky, U.S. |
Msimamo | Orthodox |
Rekodi ya ndondi | |
Jumla ya mapigano | 61 |
Ameshinda | 56 |
Alizoshinda kwa kuangusha | 37 |
Alizopteza | 5 |
Sare | 0 |
Pambano asiloshiriki | 0 |
Muhammad Ali (jina la awali: Cassius Marcellus Clay Jr.; mnamo 17 Januari 1942 - 3 Juni 2016) alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Katika mchezo wa ngumi anatazamwa kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote.
Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Roma, Italia.
Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, alikwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]
Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]
Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975.
Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uanamasumbwi, na leseni yake ya uanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.