Mvua
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mvua ni matone ya maji yanayoanguka chini kutoka mawingu angani.

Mvua ni aina ya usimbishaji. Kama matone yafikia kipenyo cha zaidi ya milimita 0.5 huitwa mvua. Kama matone ni madogo zaidi kunaitwa manyonyota. Mgongoni mwa ardhi mvua imetapaka kisawasawa.
Kutokea kwa mvua
Asili ya mvua ni mvuke wa maji katika angahewa. Kiasi cha mvuke hewani kutajwa kama gramu za maji kwa kilogramu ya hewa. [1][2] Kiasi cha unyevu (yaani maji) katika angahewa huitwa unyevuanga. Uwezo wa hewa kushika unyevuanga hutegemea halijoto ya hewa. Hewa baridi ina uwezo mdogo kutunza unyevu ndani yake, kiasi kinaongezeka kadiri halijoto iko juu zaidi. Pale ambapo hewa inafikia hali ya kushiba unyewu unaanza kutonesha yaani matone kutokea. Wakati matone yanafikia kiwango fulani cha uzito yanaanza kuanguka chini yaani mvua inaanza kunyesha.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads