Jiji la New York
jiji katika Jimbo la New York, Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jiji la New York (NYC) ni jiji kubwa zaidi nchini Marekani, liliko kusini mwa Jimbo la New York, kwenye pwani ya Atlantiki. Ni kituo cha kimataifa cha fedha, utamaduni, na diplomasia, lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 8 ndani ya jiji na zaidi ya milioni 20 katika eneo lake kuu la mji (metropolitan). Linachukua eneo la maili za mraba 468.9 (km² 1,214) na lina sehemu tano: Manhattan, Brooklyn, Queens, The Bronx, na Staten Island. NYC ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa na nyumbani kwa taasisi kubwa za kifedha, zikiwemo Wall Street na Soko la Hisa la New York.
"New York" inaelekezwa hapa. Kwa Jimbo, tazama New York (jimbo).

Remove ads
Jiografia
Mji uko kwenye mdomo wa pamoja ya mito Hudson na East River inapoishia katika Atlantiki kwa 40°42N 74°00W.
Kitovu cha mji kipo kwenye kisiwa cha Manhattan kilichopo kati ya Hudson na East River. Eneo la jiji ni funguvisiwa kwenye mdomo huo na visiwa vyake pamoja na Manhattan ni Staten Island, Long Island na visiwa vingine vidogo kwa mfano kisiwa cha Ellis na kisiwa cha Sanamu ya Uhuru (Kiingereza: "Statue of Liberty").
Jiji limepanuka kutoka kando za mito hadi barani. Eneo lote la jii ni kilomita za mraba 831.4.
Ndani ya jiji kuna mitaa au wilaya tano zinazoitwa boroughs ambazo ni:
- Manhattan (New York County)
- Brooklyn (Kings County)
- The Bronx (Bronx County)
- Queens (Queens County)
- Staten Island (Richmond County)
Remove ads
Historia

Jina la Manhattan lakumbuka wakazi asilia waliokuwa Maindio wa Lenape na "manhattan" ni neno la lugha yao "Manna-hata" lililomaaanish a "kisiwa cha milima mingi". Mzugu wa kwanza aliyefika alikuwa nahodha Mwitalia Giovanni da Verrazano mwaka 1524 halafu Mwingereza Henry Hudson mwaka 1609.
Mji mwenyewe ulianzishwa na Waholanzi kwa jina la "Nieuw Amsterdam" (Amsterdam Mpya). Mwaka 1626 kisiwa cha Manhattan kilinunuliwa kwa 60 gulder kutoka wenyeji kikawa mji mkuu wa koloni ya Nieuw Nederland (Uholanzi Mpya).
Mwaka 1664 baada ya vita kati ya Uholanzi na Uingereza koloni yote ilihamishwa upande wa Uingereza pamoja na mji mwenyewe ikapewa jina jipya la "New York".
Katika karne ya 18 New York ilikuwa sehemu ya uasi dhidi ya Uingereza
Kipindi kikubwa cha mji kulitokea katika karne ya 19 wakati wahamiaji wengi sana walipofika MArekani. Idadi kubwa walifika kwenye bandari la New York.
Baada ya fitina kati ya watu wa kusini na wenyeji wa kaskazini serikali ya Kiingereza ilifunga kambi hilo.
Remove ads
Hali ya hewa
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads