Nsunga

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Nsunga ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35316 [1].

Baadhi ya vijiji katika kata hiyo ni pamoja na:

  • Igayaza
  • Ngando
  • Omurugando
  • Byamutemba

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 26,772 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,001 waishio humo.[3]

Nsunga ni kata inayokua kwa kasi, na uchumi wake unaotegemea kilimo unakwamua watu wengi katika umaskini. Watu wanaoishi katika kata hiyo wanajihusisha na kilimo cha kahawa, ndizi, mboga, na ufugaji. Ni kata ambamo ndani yake kuna kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar, hivyo wakazi hujihusisha na kilimo cha miwa pia.

Kata hiyo imekuwa na umaarufu kwa kuwa na ukanda wenye kutuama maji, ambapo nyakati za kiangazi hutumika katika kuzalisha mboga za majani na matunda. Maeneo haya ni pamoja na Kyarukorongo, Kigwanga na Gelegele, ambako mboga nyingi huzalishwa. Wakulima hao hutegemea soko kuu la Bunazi, lililoko wilaya ya Missenyi.

Remove ads

Historia

Kata hiyo ina milima mingi ambayo ilitumika zaidi katika vita vya Kagera (1978-1979).

Tarehe 10 Septemba 2016 Nsunga ilikuwa mahali pa kitovu cha tetemeko la ardhi la Kagera 2016.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads