Oliver N'Goma

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Oliver N'Goma (23 Machi 1959 7 Juni 2010) alikuwa mpiga gitaa na mwimbaji wa muziki wa Afro-zouk na reggae kutoka nchini Gabon. Alipewa jina la utani la "Noli," alizaliwa mjini Mayumba huko mjini kusini-mwagharibi mwa nchi ya Gabon mnamo mwaka wa 1959. Alifahamika sana kwa kibao chake cha mwaka wa 1989 Bane, ambacho kilivumishwa sana na Radio Africa N.1 na Gilles Obringer.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Amekufa ...
Remove ads

Maisha na muziki

N'Goma alivutiwa kimuziki kwa mara ya kwanza na baba yake, mwalimu na mpiga harmoni. Japokuwa amepata masomo yake ya muziki kwa mara ya kwanza wakati ana umri wa miaka nane, ameanza kutumbuiza mbele ya hadhara baada ya kuhamia mjini Libreville kwa ajili ya masomo. Wakati anachukua darasa la uhasibu, amejiunga na Capo Sound, bendi ya shule, ambapo ndipo alipojifunza namna ya kupiga gitaa. Kundi lilikuwa likipiga dansi rasmi na mipira, wamefunza N'Goma sanaaa ya kutumbuiza kwenye jukwaa.

N'Goma alikuwa mwanafunzi maskini kabisa, aliyejizatiti zaidi kwenye muziki na sinema badala ya masomo. Mapenzi yake ya filamu imemwongoza hadi kufanyakazi na TV ya Gabon, ambayo imesafirisha nchini Ufaransa mnamo 1988 ambapo alijifunza kuwa mtu wa kamera.

Wakati anatumia majira ya baridi huko mjini Paris, amemaliza kazi yake ya muziki alioutunga akiwa Gabon. Ametumia pamoja muziki wake na Manu Lima, mtayarishaji wa rekodi mashuhuri kwa muziki wa Kiafrika. Lima alivutiwa sana na kazi bwana mdogo, na kushikilia mwongozo wa rekodi ya kwanza ya N'Goma iliyokwenda kwa jina la Barre.

Albamu ilifurahia mafanikio ya tabu kwa mara ya kwanza, hadi hapo kituo cha redio cha Kiafrika ilipoanza kupiga nyimbo zake. Jina la wimbo huo ilipata ushindi na mafanikio mengi huko Afrika, Ufaransa, na French West Indies, na ulienda kutamba sana katika maeneo hayo. Umefurahia mafanikio sawa tu na yale ya Mario wa Franco au Yeke Yeke wa Mory Kante. Albamu imepata kuwa moja kati ya albamu zilizouza sana katika albamu za Kiafrika hadi sasa.

N'Goma ametoa albamu ya pili, Adia mnamo Desemba 1995, amefanyakazi tena na Manu Lima. Miaka mitano baadaye, albamu yake ya tatu imetoka Seva. Kompilesheni ya vibao vikali, Best of Oliver N'Goma ilitolewa mnamo mwaka wa 2004.

Remove ads

Kifo chake

Oliver N’Goma alikufa kwa tatizo la figo kushindwa kufanyakazi vizuri, ugonjwa ambao alikuwa akipambana nao kwa takriban miaka miwili ya mwisho ya maisha yake, mnamo tar. 7 Juni 2010 kwenye Hospitali ya Omar Bongo huko mjini Libreville, Gabon, N'Goma ameiaga dunia.[1]

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads