Mnara wa taa wa Aleksandria

Mnara wa taa nchini Misri, ulijengwa karne ya 3 na kuharibiwa Zama za kati From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Mnara wa taa wa Aleksandria (pia hujulikana kama Pharos ya Aleksandria) ulikuwa mnara wa taa mjini Aleksandria huko Misri ambao ulihesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia. Kimo chake hakijulikani kikamilifu lakini kilikuwa kati ya mita 110 na 150.

Mnara huo ulijengwa kwenye kisiwa kidogo kilichoitwa "Pharos" kilichokuwa mita chache mbele ya mwambao wa Aleksandria. Baadae mnara uliitwa kwa jina la kisiwa.

Ujenzi ulitokea wakati wa utawala wa Ptolemaio II Filadelfo (280-247 KK)[1] ambapo unakadiriwa kuwa angalau ni mita 100 za urefu wa jumla.[2]. Kwa karne nyingi Pharos ilikuwa kati ya majengo marefu ya dunia. Iliporomoka baada ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea Aleksandria miaka 1303 na 1323.

Remove ads

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads