Mji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Mji ni makazi ya binadamu ambayo kwa kawaida ni makubwa zaidi kuliko kijiji lakini madogo kuliko jiji. Miji mara nyingi huwa na serikali ya mitaa iliyo wazi, na hutoa huduma za msingi na miundombinu kama vile shule, soko, na ofisi za utawala. Pia, mara nyingi huwa ni vituo vya kiuchumi na kitamaduni kwa eneo husika. Ufafanuzi halisi wa mji unaweza kutofautiana kulingana na nchi, na mara nyingi hutegemea idadi ya watu, hadhi ya kisheria, au sababu za kihistoria. Katika maeneo mengi, miji imekua kwa muda kutokana na biashara, kilimo, au viwanda, na inaweza kuendelea kukua hadi kuwa maeneo ya mijini makubwa zaidi.

Sura maalumu ya miji inategemea mambo mengi, kuanzia mazingira asili (kama yana milima, mabonde, mito, bandari n.k.).
Miji ya kwanza ilipatikana Mesopotamia, kama vile Uruk na Ur, ingawa kati ya miji inayodumu hadi leo ule wa kale zaidi labda ni Yeriko (Palestina).
Ukuaji wa madola ulifanya baadhi ya miji ipewe hadhi ya mji mkuu, kama vile Roma ambao wakati wa Yesu ulikuwa na wakazi zaidi ya nusu milioni.
Miji yenye wakazi wengi kuliko mingine ni Chongqing, Tokyo, Shanghai, Jakarta, Faiyumna na Varanasi n.k.
Africa ina miji mingi muhimu: Cairo, Lagos, Kinshasa, Johannesburg n.k.
Remove ads
Hadhi ya miji kufuatana na idadi ya wakazi
Kimataifa kulikuwa na makubaliano kwenye mkutano wa kimataifa ya takwimu ya mwaka 1887 ya kuhesabu kila mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 kama "mji mkubwa", miji kati ya wakazi 20,000 na 100,000 kama miji ya wastani na miji kati ya wakazi 5,000 na 20,000 kama miji midogo. Kufuatana na hesabu hii kulikuwa na miji mikubwa 1,700 duniani wakati wa mwaka 2002.
Katika Tanzania lugha inayotumiwa kisheria [1]ni
- Jiji ("city") kwa miji mikubwa sana
- Manisipaa ("municipality") kwa miji ya wastani
- Mji ("town") kwa miji midogo.
Mkuu wa mji huitwa mwenyekiti kwenye ngazi ya mji wa kawaida, na meya kwenye ngazi za manisipaa na jiji. Wanaongoza mikutano ya Halmashauri ya mji husika.
Remove ads
Marundiko ya mji makubwa barani Afrika
- Lagos, Nigeria milioni 21.0
- Cairo, Misri milioni 20.4
- Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo milioni 13.3
- Luanda, Angola milioni 6.5
- Nairobi, Kenya milioni 6.5
- Abidjan, Ivory Coast milioni 4.7
- Addis Ababa, Ethiopia milioni 4.6
- Johannesburg, Afrika Kusini milioni 4.4
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads