Plato
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Plato (kwa Kigiriki: Πλάτων, Platon, kumaanisha "pana, mwenye mabega mapana"; 427 KK - 347 KK) alikuwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa Ugiriki ya Kale, akiwa mwanafunzi wa Sokrates na mwalimu wa Aristoteles, wanaosemekana kuweka misingi ya kifalsafa ya ustaarabu wa Magharibi.[1].


Alibuni mawazo mengi yenye maana hadi leo. Wanafalsafa wa kisasa wamesema ya kwamba falsafa yote inamtegemea Plato.
Aliandika mafundisho yake kwa umbo la majadiliano - yaani watu wawili au zaidi wanajadili mawazo wakikubaliana au kutokubaliana nayo. Kwa njia hiyo Plato alipenda kueleza fikra zake.
Mara nyingi Sokrates ni msemaji mkuu katika majadiliano ya Plato. Huonyeshwa akiwauliza watu juu ya yale wanayoyaamini akiendelea kuuliza maswali kama mawazo yao yanalingana na mantiki. Haieleweki ni kiasi gani Plato alitumia kweli mafundisho ya Sokrates mwenyewe au kama alimtumia zaidi kifasihi kama mhusika akieleza fikra zake Plato kupitia mdomo wa Sokrates wa majadiliano.
Kati ya maandiko muhimu zaidi ya Plato ni "Politeia" yaani "kuhusu dola".
Remove ads
Dhana na vitu
Katika falsafa ya Plato kuna tofauti muhimu kati ya dhana na kitu. Dunia ya kweli ni dunia ya dhana.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads