Prince
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Prince Rogers Nelson (Juni 7, 1958 – Aprili 21, 2016) alikuwa mwanamuziki mashuhuri, mtunzi wa nyimbo, mpiga ala mbalimbali, mtayarishaji wa muziki, na mwigizaji kutoka nchini Marekani.
Remove ads
Maisha
Alizaliwa mjini Minneapolis, Minnesota. Tangu utotoni alionyesha kipaji kikubwa katika muziki. Prince alifahamika kwa sauti yake mitindo ya uvaaji. Pia alikuwa na uwezo wa kuchanganya aina tofauti za muziki kama pop, rock, funk, R&B, na soul. Mbali na kuwa na kipaji cha uimbaji, alikuwa pia mpiga gitaa, kinanda, na ala nyingine mbalimbali.
Albamu yake ya kwanza iliitwa "For You" ilitoka mwaka 1978. Hii albamu ilimtambulisha Prince kama msanii mwenye kipaji cha ajabu kwa sababu aliandika, kutayarisha, na kupiga ala zote kwenye albamu hii mwenyewe. Ingawa haikufanikiwa kibiashara kama kazi zake za baadaye, "For You" ilimpa msingi thabiti wa kufuata na kuonyesha uwezo wake mkubwa katika muziki.
Wimbo maarufu ya kwanza ya Prince ilikuwa "I Wanna Be Your Lover" kutoka kwenye albamu yake ya pili iliyotoka mwaka 1979. Wimbo huu ulifanikiwa sana na kufikia nafasi ya kwanza kwenye chati za R&B nchini Marekani, na kumfanya Prince kujulikana zaidi. Hata hivyo, kazi yake ya muziki ilipata mafanikio makubwa zaidi katika miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, hususan kupitia albamu kama "1999" (1982), "Purple Rain" (1984), na "Sign o' the Times" (1987), ambazo zilimfanya kuwa moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani.
Katika safari yake ya muziki, Prince alikumbana na changamoto mbalimbali, hususan kutoka kwa lebo ya muziki ya Warner Bros. ambayo alikuwa amesaini mkataba nayo. Kwa muda mrefu, aligombana nao kuhusu umiliki wa kazi zake na uhuru wa kisanii. Mzozo huu ulifikia kilele mwanzoni mwa miaka ya 1990, ambapo alijulikana kwa alama ya "The Artist Formerly Known as Prince" (au kifupi "TAFKAP") baada ya kuacha kutumia jina lake kwa muda. Alichora chata la neno "Slave" (mtumwa) kwenye shavu lake kama ishara ya kupinga jinsi Warner Bros. walivyomzuia kufanya kazi kwa uhuru.
Prince alifariki dunia Aprili 21, 2016, kutokana na matumizi ya juu ya dawa aina ya fentanyl, ambayo ni dawa ya maumivu yenye nguvu kubwa inayotumiwa na watu wenye maumivu makali. Upelelezi ulionyesha kuwa matumizi ya fentanyl yaliyosababisha kifo chake yalikuwa yasiyo ya kimatibabu. Kifo cha Prince kilishtua dunia nzima na kilichukuliwa kama pigo kubwa kwa tasnia ya muziki, ikizingatiwa mchango wake mkubwa na ushawishi wake kwa vizazi vya wasanii waliokuja baadaye.
Remove ads
Diskografia
Remove ads
Viungo vya nje
![]() |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads