Reli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Reli
Remove ads

Reli (kutoka Kiing. rail / railroad) ni mfumo wa usafiri wa abiria na mizigo kwa treni zinazotembea juu ya vyuma au pau za feleji. Reli ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi. Kwa maana asilia "reli" ni zile "reli za chuma" au reli za garimoshi ambazo kwa kawaida hutumiwa mbili-mbili kijozi kufanya njia ya reli yenyewe.

Thumb
Njia ya reli
Thumb
Reli ya garimoshi yenyewe
Thumb
Kituo cha reli mjini Mumbai. Reli ya Uhindi inabeba abiria milioni 17 kila mwaka [1] iko kati ya reli kubwa duniani.[2]

Kwa nchi nyingi reli ni mtindo muhimu wa usafiri kwa sababu inarahisisha mwendo wa watu na bidhaa. Ikitumiwa vema gharama zake ni afadhali kuhusu usafiri wa barabarani. Mahitaji ya nishati kwa kiwango cha mzigo ni kidogo kuliko barabarani.[3]

Faida yake ni hasa tabia za njia yake; reli za garimoshi huwa na uso tambarare isiyonyoka kwa hiyo magurudumu ya treni hutembea kwa msuguano mdogo.

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads