Riyama Ally
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Riyama Ally ni msanii wa maigizo na mwandishi na mtengenezaji wa filamu Tanzania, umaarufu wake ulitokana na kundi la sanaa la Taswira ambalo alicheza kwenye tamthilia ya ' Jabari' iliyokuwa ikionyeshwa na kituo cha luninga cha ITV.[1]
Historia
Riyama Ally ni msanii wa maigizo tangu mwaka 2000 wakati huo akiwa kwenye kundi la sanaa la Taswira, ambayo alicheza kwenye tamthilia ya Jabari kama mtoto aliyegeuzwa kichaa na mama yake ambaye alichanganya dawa alizopewa na mganga ili ampe baba yake.[1]
Mafanikio
Mwaka 2003 alijiunga na kundi la sanaa la Tamba Art Group lililokuwa likizalisha filamu za kiswahili kama ‘Miwani ya Maisha’, ‘Mzee wa Busara’ na nyinginezo nyingi ambapo yeye alicheza kwenye filamu za ‘Nsyuka’ na ‘Fungu la Kukosa’ ambazo pia ni miongoni mwa filamu zilizoandaliwa na kundi hilo.
Licha ya uigizaji wake, Riyama pia ni mtunzi wa hadithi mbali mbali za filamu moja wapo ikiwa ni hiyo yake ya ‘Mwasu’ na nyingine ambayo ameiuzia kampuni ya CB ya Charles Mokiwa, ilioko Uingereza.[1]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads