Roland Emmerich
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Roland Emmerich (amezaliwa 10 Novemba 1955) ni mwongozaji wa filamu, mwandishi-skrini, na mtayarishaji kutoka nchini Ujerumani. Anafahamika sana kwa kutengeneza filamu nyingi za majanga na mapigano. Filamu zake zimepata jumla ya mauzo zaidi ya $ bilioni 3 kwa hesabu ya dunia nzima, na kuwa zaidi ya hao wazawa wengine-waongozaji filamu kutoka barani Ulaya. Filamu zake zimepata mapato zaidi ya bilioni $1 kwa nchini Marekani, na kumfanya kuwa mwongozaji filamu wa nchini humo wa 14 kwa mapato makubwa wa muda wote.[1][2][3] Ameanza shughuri zake katika soko la filamu kwa kuongoza filamu ya The Noah's Ark Principle ikiwa kama moja ya tasnifu yake akiwa Chuo Kikuu na kuwa mmoja kati walioanzisha kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Centropolis Film Productions mnamo 1985 akiwa na dada'ke. Vilevile anafahimika kwa kuweka bayana kuwa yeye ni bwabwa.
Remove ads
Maisha ya awali na kazi
Emmerich alizaliwa mjini Stuttgart, Ujerumani na kukulia katika kitongoji cha Sindelfingen.[4] Akiwa kijana, amepata kusafiri mbali kabisa huko barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika matembezi yaliyotolewa hela na baba'ke, Hans, tajiri mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji wa mashine za bustani.[5] Mnamo mwaka wa 1977, akaanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Filamu na Televisheni cha Munich akiwa na nia ya kusomea msanifu matayarisho. Baada ya kutazama Star Wars Episode IV: A New Hope, akaamua kujiandikisha katika shule za vipindi vya uongozaji wa filamu.[6] Akatengeneza kipande kifupi cha filamu kikiwa kama hitimisho la tasnifu yake mnamo mwaka wa 1981, ametunga na kuongoza urefu mzima wa The Noah's Ark Principle, ambayo hatimaye ilichaguliwa kama filamu funguzi ya Tamasha la Filamu la Berlin la mwaka wa 1984.[7]
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads