Sakramentari

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sakramentari
Remove ads

Sakramentari (kwa Kilatini "Sacramentarium" kutoka neno "sacramentum", yaani sakramenti) ni kitabu kimojawapo cha liturujia, hasa ya Kanisa la Kilatini.

Thumb
Ukurasa wa Tyniec Sacramentary, National Library of Poland.[1]

Yaliyomo ni hasa sala inayotakiwa kusomwa au kuimbwa na askofu au padri katika Misa na ibada nyingine kadhaa, si masomo wala maneno yanayotakiwa kusomwa au kuimbwa na wengine.[2] Sehemu hizo zimo katika vitabu vingine, kama Kitabu cha Injili, Kitabu cha masomo na Graduale.[2]

Sakramentari kadhaa za zamani, hasa za mapokeo ya Roma, zinapatikana hadi leo, ama nzima ama sehemu tu. Maarufu zaidi ni zile zinazoitwa Leonianum, Gelasianum na Gregorianum.[2]

Umuhimu wake ulipungua vitabu vyote vya Misa vilipounganishwa katika misale za Karne za Kati.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads