Salami (chakula)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Salami ni aina ya soseji yenye chumvi na viungo vingi isiyopikwa ikikaushwa hewani au katika moshi baridi[1].

Asili yake iko katika nchi za Ulaya, jina limetoka katika Kiitalia kutoka Kilatini salare inayomaanisha kutia chumvi.
Salami inatengenezwa kwa kuchanganya nyama nyekundu na nyama ya mafuta baada ya kusaga yote mawili kwa vipande vidogo lakini ukubwa hutegemea aina yake[2].
Huko Italia zamani walitumia pia nyama ya punda na farasi kwa soseji hiyo lakini siku hizi mara nyingi ni nyama ya nguruwe. Kuna pia salami za nyama ya ng'ombe au nyama ya ndege kama bata mzinga au buni[3].
Kimapokeo nyama iliyosagwa na kutiwa chumvi na viungo hujazwa katika utumbo lakini siku hizi salami zinatengenezwa mara nyingi kiwandani ambako mirija ya plastiki hutumiwa.
Baada ya kujaza, aina nyingine hukaa tu hewani penye baridi ili zikauke na kuiva; aina nyingine huwekwa kwanza katika chumba chenye moshi baridi ambamo zinapokea ladha ya ziada halafu kukauka hewani.
Remove ads
Marejeo
Vungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads