Sayyid Barghash

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sayyid Barghash
Remove ads

Sayyid Barghash bin Said Al-Busaid (kwa Kiarabuبرغش بن سعيد البوسعيد; l 183726 Machi 1888), mtoto wa Said bin Sultani, alikuwa Sultani wa pili wa Zanzibar, aliyoitawala tangu tarehe 7 Oktoba 1870 hadi 26 Machi 1888.

Thumb
Barghash bin Said wa Zanzibar.
Thumb
Wanawake katika ikulu la Sultani wa Zanzibar, miaka ya 1880.

kama vile mtangulizi wake, Sayyid Bargash alijitahidi kujenga uhusiano na nchi za nje. Alifunga soko la watumwa Zanzibar mjini kulingana na mapatano ya kimataifa, lakini akavumilia biashara ya watumwa kuendelea chinichini.

Wakati wa Bargash majengo mengi ya Mji Mkongwe yakajengwa.

Barghash alikuwa na wanajeshi wa kudumu. Mwanzoni alitumia mamluki walioajiriwa kutoka Uarabuni na Uajemi, hasa Baluchistan, pamoja na watumwa[1]. Kuanzia mwaka 1877 alianzisha kikosi kipya cha askari mia kadhaa chini ya afisa Mwingereza Lloyd Mathews waliofundishwa kufuatana na utaratibu wa Kizungu; askari hao waliteuliwa chini ya Waafrika wa Unguja.[2]

Mwishowe mwa utawala wake aliona kupungukiwa kwa eneo lake kutokana na mashindano ya nchi za Ulaya ya kuenea katika Afrika baada ya mkutano wa Berlin.

Mwaka 1885 Karl Peters alifanya mikataba ya ulinzi na watawala wadogo waliokuwa chini ya Sultani barani Tanganyika. Upingamizi wa Sultani ulishindikana kwa sababu Wajerumani walituma manowari Unguja akapaswa kukubali maeneo mapya ya Wajerumani.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads