Baluchistan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Baluchistan
Remove ads

Baluchistan, Balochistan au Baluchestan[1] (بلوچستان) ni eneo linalokaliwa na Wabaluchi. Imegawiwa kati ya Pakistan, Irani na Afghanistan.

Thumb
Eneo la Wabaluchi linaonyeshwa kwa rangi ya pinki

Hapa kuna vitengo vifuatavyo:

  • Jimbo la Balochistan katika Pakistan (km² 347.190 , wakazi milioni 12.3, nusu yao Wabaluchi)
  • Mkoa wa Sistan na Baluchistan katika Irani (km² 181,785, wakazi milioni 2.5, zaidi ya nusu Wabaluchi)
  • Katika Afghanistan eneo la Wabaluchi limegawiwa kati ya wilaya za Nimruz, Helmand na Kandahar, idadi yao ni takriban 600,000.

Idadi ya Wabaluchi inakadiriwa kuwa milioni 10. Wengine huishi nje ya Baluchistan hasa katika miji mikubwa ya nchi zao. Kuna pia Wabaluchi katika Afrika ya Mashariki na mababu zao walichukuliwa kama askari na Sultani wa Zanzibar wakati wa karne ya 19.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads