Shesiafu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shesiafu
Remove ads

Shesiafu ni ndege wa jenasi Neocossyphus na Stizorhina katika familia ya Turdidae. Ndege hawa ni aina ya mikesha na waitwa pengine jina hili. Wanatokea Afrika tu. Rangi yao kuu ni rangi ya kahawia na kwa kawaida tumbo lao ni jekundu au kahawiachekundu. Hula wadudu hasa lakini wanyama wadogo wengine pia. Mara kwa mara huungana na ndege walawadudu wengine karibu na safu za siafu wakikamata wadudu na wanyama wadogo ambao wanawakimbia siafu. Lakini spishi za Stizorhina hukamata wadudu mara nyingi zaidi kama shore (kwa hivyo jina la kiingereza “Flycatcher-thrush”). Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini. Jike huyataga mayai 2-4.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads