Shinyanga (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Shinyanga ni manisipaa nchini Tanzania ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga yenye msimbo wa posta 37100. Manisipaa ya Shinyanga ni sawa na Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Remove ads
Eneo
Manispaa ya Shinyanga ina eneo la km² 548. Eneo la utawala linaundwa na jumla ya tarafa 3, kata 17,vijiji 19, mitaa 25 na vitongoji 95.
Wakazi
Kulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 161,391 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 214,744 [2].
Halihewa
Hali ya hewa ni ya kitropiki ambayo ina vipindi viwili ya majira ya mvua na kiangazi. Msimu wa mvua ni kati ya mwezi Oktoba na Desemba,pia huanza mwezi machi hadi Mei. Kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya milimita 600 hadi 1000. Kiangazi huanza mwezi Mei hadi Oktoba, pia huanza Januari hadi Februari. Wastani wa jotoridi ni kati ya nyuzi za sentigredi 18 hadi 31.[3]
Usafiri
Shinyanga huwa na kituo cha reli kwenye njia ya reli kutoka Mwanza kwenda Tabora; kwa hiyo imeunganishwa na reli ya kati Dar es Salaam - Tabora - Kigoma. Kuna uwanja wa ndege mdogo. Mji unapitiwa na barabara ya lami kutoka Mwanza kwenda Tabora.
Utamaduni
Wakazi wengi hupendelea ngoma za asili pamoja na michezo ya mbio za baiskeli, kwani ndio utamaduni wa wasukuma.
Pia, Shinyanga ni moja ya mikoa ambayo vijana wengi wako katika mrengo wa muziki wa Hip Hop, wengi wao wakifanya harakati tofauti kwa ajili ya ukombozi.
Kati ya wanamuziki maarufu wapo Noorah, Ibrah Mpanduji, na Big.com ambao wote wanafanya mahadhi ya Hip Hop.
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads