Shirika la Utalii Duniani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shirika la Utalii Duniani
Remove ads

Shirika la Utalii Duniani (kwa Kiingereza: World Tourism Organization; kifupi: UNWTO) ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa mwenye majukumu ya kukuza uwajibikaji, uendelevu na upatikanaji wa utalii (tourism). Ni shirika linaloongoza duniani kwenye sekta ya utalii ambalo linakuza utalii kama nyenzo ya kukua kwa uchumi, maendeleo jumuishi pamoja na mazingira endelevu na pia inatoa uongozi na msaada kwa sekta katika kukuza maarifa na sera za utalii duniani. Inahamasisha utekelezaji wa kanuni za kimataifa za maadili ya utalii. [1] ili kuongeza mchango wa utalii katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii huku ikipunguza athari hasi za utalii (impacts of tourism|impacts), pia kuwezesha utalii kama chombo cha kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (Sustainable Development Goals), ili kuondosha umaskini na kukuza amani duniani.

Thumb
Makao makuu ya shirika la utalii duniani,Madrid
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads