Sint Eustatius

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sint Eustatius
Remove ads

Sint Eustatius (yaani Mtakatifu Eustasi, au kifupi: Statia au Statius) ni kisiwa cha bahari ya Karibi karibu na Saint Kitts (Amerika ya Kati).

Thumb
Picha ya Sint Eustatius kutoka angani (ISS).

Ni sehemu ya pekee ya Uholanzi.[1]

Eneo lake ni kilometa mraba 21 tu.

Baada ya kuonekana na Kristofa Columbus mwaka 1493, umiliki wa kisiwa ulibadilikabadilika mara 22.

Wakazi wa kudumu ni 3,897. Wengi wao huongea hasa Krioli ya Kiingereza, ingawa Kiholanzi ndicho lugha rasmi.

Makao makuu ni Orangestad.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads