Snow White and the Seven Dwarfs (filamu ya 1937)
1937 filamu ya uhuishaji ya Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Snow White and the Seven Dwarfs (kwa Kiswahili: Mweupe Theluji na Vibete Saba) ni filamu ya katuni ya mwaka wa 1937 kutoka Marekani iliyotokana na ngano za kale ya akina Grimm, Mweupe Theluji. Ilikuwa filamu ya kwanza kuwa na kipengele kirefu katika historia ya filamu za katuni, vilevile kuwa kama filamu ya kwanza ya katuni kutayarishwa nchini Marekani, ya kwanza kutayarishwa kuwa na rangi kamili, yaani, mwanzo hadi mwisho, ya kwanza kutayarishwa na Walt Disney, na ni ya kwanza katika mfululizo wa filamu za katuni za Disney - Walt Disney Animated Classics.[2]
Snow White ya Walt Disney ilianza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Carthay Circle Theatre mnamo tarehe 21 Desemba 1937, na filamu ilitolewa katika makumbi mengine na RKO Radio Pictures mnamo tar. 4 Februari 1938. Hadithi hii imechezwa na Dorothy Ann Blank, Richard Creedon, Merrill De Maris, Otto Englander, Earl Hurd, Dick Rickard, Ted Sears na Webb Smith kutoka katika ngano za kale za Kijerumani Snow White ya akina Grimm. David Hand alikuwa mwongoza na msimamizi wa kazi hii, wakati William Cottrell, Wilfred Jackson, Larry Morey, Perce Pearce, na Ben Sharpsteen waliongoza vipengele kimoja baada ya kingine cha filamu.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads