Solon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Solon (kwa Kigiriki: Σόλων; 630 KK- 560 KK hiv) alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa serikali katika Athens kwenye Ugiriki ya Kale. Hutazamwa kama mmoja wa "Wahenga wa Kale" wa Ugiriki, kwa sababu ya matengenezo yake ya sheria za Athens. [1]
Mabadiliko mengi aliyoanzisha yalisaidia watu maskini. Alianzisha mfumo wa mahakama na majaji. Mnamo 594 KK, baraza la wazee lilimchagua Solon kuongoza Athens. Mabadiliko aliyoanzisha yalisaidia kuzuia uasi na umaskini. Kwanza alikomesha utumwa wa deni na kuwaachilia huru watu ambao walikuwa watumwa kwa sababu ya deni. Sheria yake ilikataza raia kuwa mtumwa.
Solon pia alipanga raia katika makundi manne kulingana na utajiri, sio tena ukoo na hali ya kuzaliwa kama awali. Hivyo alifungua njia kwa watu wapya kufikia kwenye uongozi.
Solon aliruhusu raia wote kuhudhuria mkutano wa wananchi na kushiriki katika uchaguzi wa viongozi. Sheria zake zilipunguza ukali wa adhabu.
Remove ads
Marejeo
Bibliografia
Mengineyo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads