Sweet Fanta Diallo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
"Sweet Fanta Diallo" ni jina la wimbo ulioimbwa na kutungwa na mwanamuziki wa miondoko ya reggae kutoka nchini Ivory Coast, Alpha Blondy. Wimbo unatoka katika albamu ya Revolution iliyotoka mwaka 1987.[1][2] Ndani ya wimbo, Alpha alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia na kulazwa katika moja ya hospitali huko nchini Ivory Coast. Alipata tiba na kupona kwa asilimia mia moja. Siku moja alifikiria kurudi pale hospitalini kwa minajili ya kutoa shukrani kwa nesi mrembo sana aliyemsimamia hadi kupona aliyetambulika kwa jina la Fanta Diallo. Matokeo yake ya kwenda kutoa shukrani kwa nesi huyo yaliishia butwaani baada ya kuambiwa ya kwamba hakuna nesi mwenye jina hilo katika hospitali ile. Imani yake iliendelea kumwambia ya kwamba yule alikuwa malaika na si mwanadamu kabisa.[3]
Remove ads
Orodha ya nyimbo
Kwenye santuri ya wimbo huu kuna nyimbo mbili.
Tazama pia
- Revolution
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads