Ulinganifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ulinganifu (pia: mpachano[1], ing. symmetry ) ni tabia ya maumbo na magimba yenye sehemu zinazolingana. Kama sehemu za kitu ni kama pacha zinaitwa linganifu.

Miili ya viumbehai wengi inafuata muundo wa ulinganifu kwa sababu macho, masikio, mikono, miguu na viungo vingine (si vyote!) viko mahali sawa upande wa kushoto kama upande wa kulia. Hii ni kama taswira geu inayoakisiwa. Mfuno huu unaweza kuitwa ulinganifu wa mstari[2] kwa sababu sehemu pacha ya geu inatokea kwenye mstari wa kioo au jira ya ulinganifu.
Kuna mfumo wa pili unaofuata nukta ya ulinganifu (pia: nukta ya pacha[3]). Hapo pande mbili zina umbali sawa na kitovu ambacho ni nukta ya ulinganifu.
Remove ads
Mifano ya maumbo linganifu
- Maumbo linganifu na jira za ulinganifu
- Umbo lenye mfumo wa ulinganifu wa nukta ("Zentrum" = Kitovu")
- Ulinganifu wa nukta kwamfano wa kiti cha pweza
- Ulinganifu katika sanaa (mchoro wa Leonardo da Vinci)
- Ulinganfu katika usanifu majengo
Marejeo
Kujisomea
Viungo ya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads