Mkono

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkono
Remove ads

Mkono ni kiungo cha mwili kinachoanza penye bega na kuishia penye kiganja na vidole. Huwa na sehemu mbili ambazo ni mkono wa juu na kigasha zinazounganishwa kwa kiwiko au kisugudi.

Thumb
Sehemu za mkono

Mkono huishia kwa vidole vitano ambavyo ni: kidole gumba[1], kidole cha shahada, kidole cha kati, kidole cha pete na kidole cha mwisho. Vidole vyote huweza kufanya kazi pamoja.

Thumb
Mifupa ya mkono wa kibinadamu

Miongoni mwa wanadamu, mkono ni kiungo kilichotokea kutokana na mabadiliko ya miguu ya mbele ya mamalia wengine. Mikono inafanya pia kazi muhimu katika lugha ya mwili na lugha ya ishara.

Remove ads

Tanbihi

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads