Tabenakulo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tabenakulo ni sanduku imara la kuhifadhia sakramenti ya ekaristi katika baadhi ya madhehebu ya Ukristo, hasa Kanisa Katoliki, la Kiorthodoksi na ushirika wa Anglikana na pengine hata kati ya Walutheri.




Desturi hiyo inategemea imani kuhusu Yesu Kristo kuendelea hata baada ya Misa kwisha kuwemo katika mkate uliowekwa wakfu.
Lengo la kutunza hiyo sakramenti inayosadikiwa kuwa "Mwili wa Kristo" ni kuweza kuipeleka kwa wagonjwa wasioweza kushiriki Misa yenyewe.
Hata hivyo, kwa kuwa Wakristo hao wanaamini humo ndani Yesu yumo, tabenakulo inakuwa kivutio hasa kwa sala binafsi.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads