Tarzan (filamu ya 1999)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Tarzan ni filamu ya katuni ya mwaka 1999 iliyodhaminiwa na Walt Disney kwa ajili ya Walt Disney Pictures. Inahusu historia ya Tarzan of the Apes iliyotolewa na Edgar Rice Burroughs. Hii ni filamu ya 37 kutolewa katika mfululizo wa filamu za Walt Disney Animated Classics.

Ukweli wa haraka Imeongozwa na, Imetayarishwa na ...
Remove ads

Muhtasari wa hadithi

Filamu hii inahusu mtoto mdogo aliyelelewa na kundi la sokwe walio msituni baada ya mtoto wao wa halisi kuliwa na chui. Katika katuni hii mtoto huyu anarithishwa jina la Tarzan. Tarzan amekuwa akiishi vizuri na wanyama wengine wote bila ya kujua kuwa baba yake bandia ambaye ni sokwe alimchukia kwa sababu ya kuwa Tarzan siyo mtoto wake wa halisi. Madhumuni makuu ya filamu hii yanaanza ambapo Tarzan anakutana na msichana anayetokea mjini pamoja na baba yake na mlinzi wao. Baada ya Tarzan kukutana na binti huyo ndipo anapoanza kujifunza zaidi maisha ya mjini. Hapa ndipo Tarzan ana gundua ya kwamba yeye si kizazi cha sokwe bali ni kizazi cha binadamu. Lakini baadaye wanakuja kugundua ya kwamba mlinzi wa yule binti ana njama za kuteka wanyama wa msituni pamoja na kumteka Tarzan pia. Lakini Tarzan anajaribu kila anachokiweza na kwa ushirikiano wa binti yule na baba yake pamoja na wanyama wengine Tarzan anafanikiwa kumshinda yule mlinzi na kuhakikisha usalama wa wanyama wote wa msituni.[2]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads