Tekineti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tekineti (kutoka Kigiriki τεχνητός teknitos "bandia") ni elementi sintetiki na metali. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Tc na namba atomia 43 katika mfumo radidia.

Remove ads
Tabia
Tekineti hupatikana kwa maumbo mbalimbali. Ikitokea kama vumbi ina rangi ya majivu. Ikitokea kama metali imara hufanana na platini.
Ni elementi nururifu inayopatikana kwa kawaida kama elementi sintetiki inayotengenezwa kwa matumizi yake. Hutokea pia kiasili kwa viwango vidogo sana katika mbunguo wa urani.
Isotopi
Isotopi inayopatikana zaidi ni 99mTc yenye nusumaisha ya miaka 211. Hutumiwa katika tiba kwa uchunguzi wa mwili hasa uaguzi wa kansa.
Historia
Kuwepo kwa elementi hii kulitabiriwa na Mendeleev tangu karne ya 19. Ilitambuliwa mara ya kwanza 1925 Ujerumani lakini jaribio halikuweza kurudiwa.
Mwaka 1937 ilipatikana kwa njia iliyokubaliwa na umma wa sayansi kwenye chuo kikuu cha Palermo (Sisilia - Italia). Emilio Segrè na Carlo Perrier walipata elementi mpya katika ubamba wa Molibdeni uliowahi kupigwa kwa mnururisho wa kinyuklia. Hii ilikuwa elementi sintetiki ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu. Wafumbuzi wakatoa jina la "technetium" kutokana na neno la Kigiriki kwa "bandia".
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tekineti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads