The Fox and the Hound

From Wikipedia, the free encyclopedia

The Fox and the Hound
Remove ads

The Fox and the Hound (kwa Kiswahili: Mbweha na Mbwa wa Kuwinda) ni filamu ya katuni iliyotolewa mnamo mwaka 1981. Filamu ilitayarishwa na Walt Disney Productions, na kutolewa kwenye kumbi za filamu tarehe 10 Julai 1981 na Buena Vista Distribution. Hii ni filamu ya ishirini na nne kutolewa katika mfululizo wa Walt Disney Animated Classics, na inatokana na kitabu cha Daniel P. Mannix chenye jina sawa na la filamu hii, na inahusu urafiki wa mbweha Tod na mbwa Copper.

Ukweli wa haraka Imeongozwa na, Imetayarishwa na ...

Nyota wa filamu hii waliotia sauti zao ni pamoja na Mickey Rooney, Kurt Russell, Pearl Bailey, Jack Albertson, Sandy Duncan, Jeanette Nolan, Pat Buttram, John Fiedler, John McIntire, Dick Bakalyan, Paul Winchell, Keith Mitchell, na Corey Feldman. Wakati wa kutolewa, ilikuwa ghali zaidi filamu ya katuni zinazozalishwa, kugharimu $12 milioni.[1] Ikafuatiwa na filamu, The Fox and the Hound 2, ilitolewa na DVD mnamo tarehe 12 Desemba 2006.

Remove ads

Hadithi

Filamu inaanza na mtoto wa mbwa mwitu ambaye amebaki yatima baada ya mama yake kuuawa na wawindaji. Bundi mmoja aitwaye Big Mama pamoja na marafiki zake wawili—ndege mdogo aina ya shomoro anayeitwa Dinky na ndege mwingine mkubwa aitwaye Boomer—wanapanga mpango wa kumpeleka mtoto huyo kulelewe na mjane mmoja anayeitwa Bi Tweed. Bi Tweed anampatia mtoto huyo jina la Tod, na anaanza kumlea kwa upendo na kumfundisha jinsi ya kujitegemea.

Wakati huo huo, jirani wa Bi Tweed, mwindaji anayeitwa Amos Slade, anamleta nyumbani mbwa wake mchanga aitwaye Copper na kumtambulisha kwa mbwa wake mkubwa wa uwindaji aliyeitwa Chief. Hapo ndipo urafiki wa ajabu unapoanza kati ya Tod na Copper, ambapo wanaapa kuwa "marafiki milele."

Hata hivyo, Amos Slade anakasirishwa na tabia ya Copper ya kucheza kila mara na Tod, hivyo anamfungia nyumbani. Siku moja, Tod anapomtembelea Copper nyumbani, anamwamsha Chief bila kujua. Slade na Chief wanamkimbiza Tod, lakini Bi Tweed anawazuia.

Baada ya ugomvi mkali, Slade anaapa kwamba atamwua Tod kwa vyovyote vile. Msimu wa uwindaji unapoanza, Slade anaondoka na mbwa wake kwenda porini. Wakati huo, Big Mama anamshauri Tod kwamba urafiki wake na Copper hauwezi kudumu, kwa sababu wao ni maadui wa kiasili. Lakini Tod anakataa kuamini hilo.

Miaka inapita, na sasa Tod na Copper wamekuwa watu wazima. Usiku mmoja, Tod anampata Copper akirudi nyumbani na kumwuliza kama bado wanaweza kuwa marafiki. Copper anamjibu, "Nyakati hizo zimepita. Sasa mimi ni mbwa wa kuwinda."

Copper anamwonya Tod kuwa Chief anaweza kuamka, lakini Tod anasema haogopi. Chief anaamka na kumwamsha Slade. Wakamkimbiza Tod, lakini Copper anamwokoa kwa kuwapotosha Slade na Chief ili Tod atoroke. Tod anajaribu kutoroka kupitia njia ya reli, lakini kwa bahati mbaya Chief anamuona na kumkimbiza hadi gari moshi linapomgonga Chief. Slade na Copper wanamlaumu Tod na kuapa kulipiza kisasi.

Bi Tweed anatambua kuwa hawezi tena kumlinda Tod, hivyo anampeleka msituni. Huko msituni, Big Mama anamkutanisha Tod na mbweha wa kike aitwaye Vixey, na maisha yanaanza kuonekana mazuri tena. Lakini Slade na Copper wanafuatilia hadi kwenye hifadhi hiyo na kuanza kuwawinda.

Wakati Slade anapanga kuwapiga risasi, ghafla dubu mkubwa anajitokeza na kumshambulia. Slade anakimbia na kuangukia kwenye mtego wake mwenyewe huku silaha yake ikitupwa mbali. Copper anajaribu kupambana na dubu, lakini hana nguvu ya kutosha. Tod anajitokeza na kupambana na dubu kwa ujasiri, hadi wote wanaanguka kwenye maporomoko ya maji.

Baada ya hapo, Copper anamshauri Tod ajifanye amelala ili asipigwe risasi na Slade. Slade anapojitokeza tayari kwa risasi, Copper anasimama mbele ya Tod kumzuia asipigwe. Hatimaye, Slade anashusha bunduki yake na kuwaacha wawili hao kwa amani, japokuwa bado kuna ukakasi kati yao.

Nyumbani, Bi Tweed anamsaidia Slade kupona wakati mbwa wake wanapumzika. Copper, kabla hajalala, anatabasamu akimkumbuka rafiki yake wa utotoni. Kwenye kilima jirani, Tod na Vixey wanaonekana wakimtazama Copper na Bi Tweed kwa utulivu, wakifurahia maisha mapya, huku kumbukumbu za urafiki wao wa ajabu zikibaki milele.

Remove ads

Washiriki

  • Mickey Rooney kama Tod
  • Kurt Russell kama Copper
  • Pearl Bailey kama Big Mama
  • Jack Albertson kama Amos Slade
  • Jeanette Nolan kama Widow Tweed
  • Pat Buttram kama Chief
  • Keith Mitchell kama Young Tod
  • Corey Feldman kama Young Copper
  • Sandy Duncan kama Vixey
  • Paul Winchell kama Boomer
  • Dick Bakalyan kama Dinkey
  • John Fiedler kama Porcupine
  • John McIntire kama Badger

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads