The Italian Job

From Wikipedia, the free encyclopedia

The Italian Job
Remove ads

The Italian Job ni filamu ya mwaka 2003 yenye vituko-kupigana. Filamu iliongozwa na F. Gary Gray, na nyota wa filamu ni Jason Statham, Mark Wahlberg, Charlize Theron, Edward Norton na Donald Sutherland. Filamu inarejea jina sawa na ile filamu halisi ya awali iliyochezwa na nyota Michael Caine kunako miaka ya 1969.

Ukweli wa haraka
Remove ads

Njama

Muhtasari wa filamu

Filamu inaazia mjini Venice, Italia, tunakutana na kiongozi wa wanakikosi cha filamu hii Bw. John Bridger (Donald Sutherland) akiwa anampigia simu binti yake aitwae Stella (Charlize Theron) huku baba wa binti huyo akimweleza mwanae kwamba "hii ndiyo kazi yangu ya mwisho" (mazungumzo kupitia simu).

John kisha akakutana mmoja kati ya wanamipango wenzi "mzee wa kazi" Charlie (Mark Wahlberg) ili kujadiliana kuhusu mipango ya kazi. John na Charlie ni washikaji sana, na wawili hao wanaheshimiana kwa kiasi kikubwa kabisa.

Baada ya hapo Charlie akapanga mpango wa kuweza kuiba kijumbamshale chenye fito za dhahabu ndani yake. Kweli mpango ulifana. Baada ya mpango kukamilika, ikabidi wanakundi wote wakutane kivukoni ili kuweza kujua nini kitakacho endelea baada ya mpango kufanikiwa.

Haya, mpango ulifaulu na sherehe zikaanza juu ya ushindi huo, lakini shangwe hizo hazikudumu kwa muda mrefu kwani mmoja kati ya wanakundi akawasaliti wenziwe (Steve) alikuwa na mpango wake binafsi, na hakupoteza muda kwa kuisubira dhahabu hiyo, akamwua Bridger, kisha akaondoka zake huku akiliacha kundi likiwa taabani. Kwa bahati nzuri waliponyeka, na wakaanza kupanga mpango mwingine wa kulipiza kisasi dhidi ya kitendo alicho kifanya Steve (Edward Norton).

Remove ads

Washiriki

Maelezo zaidi Mwigizaji, Jina alilotumia ...

Marejeo kwa Kiingereza

  1. http://www.boxofficemojo.com/movies/?id=italianjob.htm
  2. http://au.rottentomatoes.com/m/italian_job/ Ilihifadhiwa 23 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
  3. http://www.metacritic.com/movie/the-italian-job
  4. http://www.imdb.com/title/tt0317740/awards

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads