Mos Def
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dante Terrell Smith (amezaliwa tar. 11 Desemba 1973) ni jina la kutaja mwigizaji na MC kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mos Def na Yasiin Bey. Alianza kazi zake muziki wa hip hop akiwa na kundi la Urban Thermo Dynamics, ambamo aliweza kuonekana katika albamu za Da Bush Babees na De La Soul.
Akiwa na Talib Kweli, ameanza kundi la Black Star, kundi ambalo limetoa albamu ilkiyokwenda kwa jina la Black Star mnamo mwaka wa 1998. Alikuwa chachu kubwa wa hip hop chipukizi wa miaka mwishoni mwa miaka ya 1990 wakati yupo na studio ya Rawkus Records.
Akiwa kama msanii wa kujitegemea, amefanikiwa kutoa albamu kadhaa ambazo ni Black on Both Sides mnamo 1999, The New Danger mnamo 2004, True Magic mnamo 2006, na The Ecstatic iliyotoka mnamo mwaka wa 2009.[1]
Ijapokuwa awali alitambulika kwa kazi zake za muziki ambazo amezitoa, lakini tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, kazi nyingi za Mos Def katika chideo zimemfanya awe rapa pekee aliyeweza vyema katika kazi zake za uigizaji. Anafahamika zaidi kwa kucheza kwake kama Brother Sam katika igizo la Kimarekani la Dexter. Mos Def amekuwa akijishughulisha mara kwa mara katika masuala ya kijamii na kisiasa.
Remove ads
Diskografia
- Black on Both Sides (1999)
- The New Danger (2004)
- True Magic (2006)
- The Ecstatic (2009)
- Yasiin Bey Presents (TBA)[2]
- Kolabo alizofanya
- Mos Def & Talib Kweli are Black Star (1998) (akiwa na Talib Kweli kama Black Star)
- Black Star Aretha (2012) (akiwa na Talib Kweli kama Black Star)[2]
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads