Thenashara

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Thenashara (pia thinashara) ni Kiswahili cha pwani kwa ajili ya namba kumi na mbili (12).

Asili ni Kiarabu "اثنا عشر" (ithnayn `ashara - ithnashara).

Kwa Kiswahili sanifu "kumi na mbili" imechukua nafasi yake lakini bado hutumika.

Thenashara katika Biblia

Katika tafsiri kadhaa za Biblia "Thenashara" inamaanisha hasa Mitume wa Yesu kumi na wawili pale ambapo neno la Kigiriki "dodeka" (=12) linatumiwa kama jina si namba.

Toleo la Biblia (Union Version) linatumia "wale Thenashara" pale ambako Kigiriki asilia cha Agano Jipya kinasema "οἱ δώδεκα" (hoi dodeka) [1]. Pale ambako lugha asilia inatumia "dodeka" kama namba Kiswahili cha Union Version kinatumia "kumi na wawili".[2]

Matoleo mengine ya Biblia, kwa mfano Habari Njema kwa watu wote, hutumia "kumi na wawili" kote.

Remove ads

Thenashara katika Uislamu

Wakati mwingine Thenashara inaweza kumaanisha madhehebu ya Shia katika Uislamu ambalo mara nyingi kwa Kiarabu huitwa "Ithnashara" kutokana na maimamu 12 wanaoheshimiwa. Ni kundi kubwa kati ya Washia hasa nchini Uajemi, Irak na Lebanon.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads