Udongo kinamo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Udongo kinamo
Remove ads
Remove ads

Udongo kinamo (pia: udongo wa kinamu, udongo wa mfinyanzi; kwa Kiingereza: clay) ni aina ya udongo ambao una chembechembe ndogo sana na una tabia ya kushikamana.

Thumb
Udongo wa kinamu nchini Estonia

Udongo wa aina hiyo huwa na uwezo mkubwa wa kushika maji ndani yake. Ganda la udongo kinamo, tofauti na mchanga, haupitiwi na maji kwa urahisi.

Udongo kinamo huwa mgumu ukikauka kabisa. Tangu miaka elfu kadhaa ulitumiwa na binadamu kwa kufinyanga vyombo. Maana udongo huo ukiwa katika hali mbichi unakubali umbo lolote linalopewa na mfinyanzi. Kama unachomwa, yaani kuokwa katika tanuri kwa joto la sentigredi 1000 au zaidi, tabia yake inabadilika. Huwa mgumu, na haubadilishwi tena na maji. Vitu kama matofali ya ujenzi na vyombo kama sahani, vyungu au sufuria hutengenezwa kwa njia hiyo ambavyo vinaweza kudumu miaka mingi visipovunjwa.

Remove ads

Marejeo

Loading content...

Kujisomea

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads