Ujerumani Magharibi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ujerumani Magharibi
Remove ads

Ujerumani Magharibi (kwa Kiingereza: West Germany) ilikuwa jina lililotumika kuelezea Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani kati ya miaka ya 1949 hadi 1990, kabla ya kuungana kwake na Ujerumani Mashariki. Wajerumani wengi hawakupenda jina hili kwa sababu katika lugha ya Kijerumani ni jina la kijiografia kwa kutaja eneo la magharibi la nchi hasa maeneo karibu na mto Rhine. Watu wa kusini na kaskazini kama wakazi wa Bavaria au Hamburg hawakujisikia kama "Wajerumani ya Magharibi".

Thumb
Ujerumani, kanda za utawala wa washindi wa Vita Kuu ya Pili mwaka 1946
Thumb
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani 1949 - 1990

Iliundwa baada ya Vita Kuu vya Pili vya Dunia katika maeneo yaliyokuwa yakikaliwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa. Mji mkuu wake ulikuwa Bonn, hivyo wakati mwingine uliitwa "Jamhuri ya Bonn".[1]

Wakati wa vita baridi, Ujerumani Magharibi ilikuwa sehemu ya kambi ya Magharibi na mwanachama wa NATO. Uchumi wake ulikua kwa kasi kubwa katika miaka ya 1950, kipindi kilichoitwa Wirtschaftswunder (muujiza wa kiuchumi). Chansela wa kwanza, Konrad Adenauer, alihimiza uhusiano wa karibu na nchi za Magharibi na ushirikiano wa Ulaya.[2]

Kanda la Kirusi la Ujerumani ilikuwa dola la pili katika Ujerumani kwa jina la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani.

Mnamo 1990, baada ya kuporomoka kwa Ukuta wa Berlin na kuanguka kwa mfumo wa kikomunisti Ulaya Mashariki, Ujerumani Mashariki iliungana rasmi na Ujerumani Magharibi mnamo 3 Oktoba 1990, kuunda taifa moja la Ujerumani ya leo.[3]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads