Ukatekumeni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ukatekumeni (kutoka neno la Kigiriki κατηχούμενος, katēchúmenos, yaani "mtu anayefundishwa", kwa Kiingereza "catechumen") ni kipindi cha malezi ya Kikristo ambacho kinalenga hasa kuandaa watu kwa ajili ya ubatizo.

Kadiri ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, uliorudisha katika Kanisa Katoliki taratibu za karne za kwanza baada ya Kristo, ni kwamba, kisha kuchunguza na kunyosha sababu za uongofu wao, waliojaliwa mwanzo wa imani wapokewe kwa ibada maalumu katika ukatekumeni ambao ufuate maagizo mbalimbali ya sheria za Kanisa [1].
Madhehebu mengine ya Ukristo, kama Waanglikana [2] Walutheri,[3] Wamethodisti,[4] Waorthodoksi, Wakalvini,[5], ingawa si yote, yana utaratibu wa namna hiyo.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
