Umbile
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Umbile (kwa wingi: Maumbile) ni neno linaloendana na neno "umbo" na kutokana na kitenzi "kuumba". Umbile ni hali inayoelezea kitu fulani kilivyo.


Katika kuelezea kitu hicho kila mtu huwa na mtazamo wake, yaani: kuna atakayesema "kitu kile ni kikubwa", mwingine atasema "kitu kile ni kidogo" na mawazo mengine tofautitofauti, kama vile "kitu kile ni kizuri", "kitu kile hakifai", n.k.
Mfano: Tukizungumzia umbile la mbwa tutasema:
- Mbwa ni mnene ama
- Mbwa ni mwembamba.
Pia:
- Mbwa ni mfupi ama
- Mbwa ni mrefu
Mfano mwingine: Tukizungumzia kuhusu umbile la nyoka tutasema:
- nyoka ni mfupi ama
- nyoka ni mrefu
Pia:
- nyoka ni mnene ama
- nyoka ni mwembamba
Sayansi mbalimbali zinachunguza umbile upande mmoja na kwa vigezo vyake, falsafa upande mwingine kwa kutumia hasa hoja za mantiki n.k.
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
