Ungamo la Augsburg

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ungamo la Augsburg
Remove ads

Ungamo la Augsburg ni mafundisho yaliyotungwa mwaka 1530 na wafuasi wa Martin Luther walipodaiwa kujieleza mbele ya Bunge la Dola Takatifu la Kiroma ili kurudisha umoja wa Kanisa[1].

Thumb
Bunge la Augsburg kadiri ya Christian Beyer.

Lengo lake lilikuwa kuendeleza matengenezo ya Kiprotestanti, lakini pia kudumisha umoja huo.

Katika sehemu ya kwanza (1-21) linafafanua mafundisho ya Kilutheri namna ya kuonyesha kwamba hayapingani na yale ya «Kanisa Katoliki au ya Kanisa la Roma».

Sehemu ya pili inazungumzia mabadiliko yaliyoanzishwa na watengenezaji ili kurekebisha mambo kadhaa yaliyotazamwa kama «maovu» (22-28), ikieleza haja ya mabadiliko hayo.

Ungamo hilo ni thibitisho tosha la nia ya Walutheri wa kwanza ya kubaki ndani ya Kanisa pekee linaloonekana.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads