Uzuri

From Wikipedia, the free encyclopedia

Uzuri
Remove ads

Uzuri ni sifa ya nafsi, mnyama, mahali, tendo, wazo, neno, tungo, sauti, picha au kitu chochote kinachopendeza.

Thumb
Anga katika Atacama Desert. Uzuri wa uasilia umekuwa mara nyingi kichocheo cha usanii wa binadamu.


Thumb
Pambo la maua, Jin Dynasty (11151234 BK), Shanghai, China.
Thumb
Dirisha la rangi katika kanisa la Notre Dame de Paris, Ufaransa. Katika sanaa ya Kigothi, nuru ilitazamwa ufunuo wa kwanza wa Mungu.
Thumb
Kuba la Kanisa kuu la Florence. Kuanzia tapo la Renaissance huko Ulaya, ulinganifu na uwiano wa vipimo vilitazamwa vya msingi katika suala la uzuri.

Kimsingi, kwa wanaomuamini Mungu, ni sifa yake ambayo inajumlisha zile za umoja, ukweli na wema, na kujitokeza katika utakatifu wa watu wake.

Kwa namna mbalimbali uzuri unachunguzwa na falsafa, sosholojia, saikolojia n.k. na kulengwa na binadamu tangu zamani za kale, hasa kwa njia ya sanaa za aina mbalimbali. Tangu mtu yupo, hawezi kuridhika na mahitaji ya mwili tu.

Pengine uzuri unategemea utamaduni, lakini mara nyingi unapendeza watu wote.

Mang'amuzi ya "uzuri" mara nyingi yanatokana na utambuzi wa ulinganifu na uasilia, unaomfanya mtu ajisikie salama na kuridhika.

Hata hivyo, kwa kuwa mara kadhaa ni mang'amuzi ya binafsi, mithali ya Kiingereza inasema, "beauty is in the eye of the beholder" ("uzuri umo jichoni mwa mtazamaji")[1]hata pengine ni suala la urithi.[2][3]

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads