Ustahimilivu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ustahimilivu (kutoka kitenzi cha Kiarabu) ni mchakato na uwezo wa kukabiliana na mambo magumu na changamoto za maisha, kulingana na ufafanuzi kutoka Chama cha Kisaikolojia cha Marekani (APA). Ustahimilivu unamaanisha kubadilika kiakili, kihisia, na kitabia na uwezo wa kuzoea mabadiliko husika yalikufika[1].
"Ni uwezo wako wa kustahimili shida na kukua licha ya changamoto za maisha[2]," anasema Amit Sood, MD, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Ustahimilivu na Ustawi na mmiliki wa mpango wa Chaguo Resilient.
Ni muhimu kutambua kwamba kuwa mstahimilivu kunahitaji seti ya ujuzi ambao unajengeka kwa muda. Kujenga uthabiti kunahitaji muda, nguvu, na usaidizi kutoka kwa watu walio karibu yako. Kuna uwezekano pia utapata vikwazo njiani. Inategemea tabia na ujuzi wa mtu bibinafsi, kama kujipenda na uwezo wa kufanya mawasiliano na wengine kuhusu tatizo linalokusibu. Sababu zinazoweza kuchangia mtu kuwa mstahimilivu ni pamoja na usaidizi wa kijamii na rasilimali zinazopatikana kwa wakati huo.
Kuwa mstahimilivu hakumaanishi kwamba hupati wasiwasi, kuumia kihisia, au kuteseka. Kuonyesha uthabiti/ustahimilivu ni pamoja na kufanya kazi katika hali ya maumivu ya kihisia na mateso[3].
Mstahimilivu ni mtu ambaye ana ujuzi thabiti wa kukabiliana na hali hiyo na anayeweza kutumia rasilimali zake zilizopo, kuomba msaada inapohitajika, na kutafuta njia za kudhibiti hali inayomkabili[4]. Watu walio na ustahimilivu wa kisaikolojia wanaweza kutumia ujuzi na nguvu zao kukabiliana na changamoto za maisha kama vile:
- Kifo cha mpendwa
- Talaka
- Masuala ya kifedha
- Ugonjwa
- Kupoteza kazi
- Uhitaji wa matibabu
- Majanga ya asili
Badala ya kukata tamaa au kutumia mikakati isiyofaa ya kukabiliana na hali hiyo, watu wenye ustahimilivu hukabiliana na magumu ya maisha kwa kusubiri, kujiamini na kuamini kwamba hili nalo litapita.
Ikiwa unatatizika kukabiliana na changamoto, usiogope kuzungumza na mtu ambaye una hakika unamuamini au mtaalamu wa afya ya akili. Hata watu wastahimilivu wanahitaji usaidizi na sehemu ya kuwa mstahimilivu ni kujua wakati wa kuomba msaada[5]
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads