Kimelea
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kimelea (pia: kidusia[1]; kwa Kiingereza parasite) ni kiumbehai ambaye anaishi ndani au juu ya kiumbehai mwingine wa spishi tofauti na kupata virutubishi kutokana na mwili wa kiumbe huyo, ambaye kwa kawaida ni mkubwa zaidi, bila kumpa kiumbe mwenyeji faida yoyote. Kinyume chake, mara nyingi analeta hasara au kusababisha ugonjwa.

Vimelea vingi ni vidogo sana vikiishi ndani ya wanyama au binadamu.
Remove ads
Aina za vimelea
Vimelea vingine ni vikubwa kiasi cha kuonekana kwa jicho:
- minyoo inayoishi ndani ya utumbo kama mategu na nematodi nyingine
- chawa na viroboto vinavyokaa juu ya ngozi na kunyonya damu
Vimelea vingine ni vidogo mno, vinaonekana kwa hadubini tu:
Remove ads
Vimelea kati ya mimea na wanyama
Kuna pia wanyama wakubwa zaidi wanaotumia mbinu za kimelea kwa mfano ndege kama vile kekeo, fumbwe au kinili wanaotega mayai katika matego ya spishi nyingine.
Kuna mimea inayopata lishe kwa kutumia moja kwa moja majimaji ya mimea mingine na aina kadhaa kati ya hizi zinaendelea bila kutumia usanisinuru kabisa.
Vimelea na wenyeji wao
Vimelea mara nyingi hudhoofisha viumbehai wenyeji wao vinamoishi na vinaweza kusababisha magonjwa; kwa kawaida haviwaui mara moja, maana kimelea kinachomwua mwenyeji wake kitakosa mahali pa kuishi.
Vimelea vingi vinahitaji mazingira ya mwili wa spishi fulani vikiweza kuishi hapo tu.
Vimelea nje ya mwili wa mwenyeji
Vimelea hawa ni kama chawa, kunguni na kupe ambao huishi nje ya mwili wa mwenyeji (ecto-parasites) na hufyonya damu na kutaga mayai juu yake. Huenda wakasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Wao hungojea mwenyeji aje karibu nao ambapo wanamnata na kuanza kumtegemea kwa lishe na pia kwa pahala pa kuzalisha.
Marejeo
Kujisomea
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads