Kiongozi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kiongozi
Remove ads

Kiongozi ni mtu ambaye huongoza wa wenzake, ama mmojammoja ama katika kikundi.

Thumb
Julius Caesar, mmojawapo kati ya viongozi maarufu zaidi katika historia.

Mara nyingi kiongozi hupewa heshima ya juu katika jamii au kikundi cha watu kuanzia katika familia ambapo huheshimiwa na wote katika eneo husika analolisimamia.

Kiongozi katika familia

Kiongozi katika familia huwa ni mtu aliye na umri mkubwa katika familia husika, ambapo viongozi huwa ni baba na mama. Katika familia nyingi baba ndio huwa kiongozi mkubwa akifuatiwa na mama.

Pia familia huweza kuwa na kiongozi wa ukoo ambapo bibi na babu huwa viongozi wa juu katika ukoo.

Kiongozi katika jamii

Katika nchi nyingi duniani kiongozi hupatikana kwa wananchi kupiga kura ambapo watu mbalimbali wanaogombea uongozi hupigwa kura kwa ajili ya kuwa kiongozi katika jamii au kikundi cha watu hupatikana.

Mara nyingine kiongozi huchaguliwa kwa kuteuliwa na mtu mmoja pasipo kupigwa kura.

Pia katika jamii nyingine kiongozi hupatikana kwa kurithi, ambapo mrithi huwa kiongozi kwa kurithi uongozi kutoka kwa kiongozi aliyefariki na kuachia madaraka.

Remove ads

Kiongozi kadiri ya Biblia

Katika Biblia kiongozi ni mtu ambaye humwakilisha Mungu katika kuongoza watu wake hapa duniani[1]. Hivyo anapaswa kukumbuka kwamba ameshirikishwa mamlaka ya juu na kwamba atapaswa kuhukumiwa kwa namna alivyoitumia.

Yesu alisema kwa kawaida watawala hutumia mabavu na hata hivyo hupenda kuitwa wafadhili.

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads