Vitamini C

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vitamini C
Remove ads
Remove ads

Vitamini C ni vitamini inayopatikana hasa katika matunda na majani mabichi. Kikemia ni aina ya asidi askobini na binadamu ni kati ya spishi chache ambazo haziwezi kutengeneza asidi hii mwilini. Kwa hiyi watu hutegemea chakula chenye kiwango cha vitamini hii.

Thumb
ascorbic acid
Thumb
Viazi katika ganda huwa na 20 mg/100 g za vitamini C

Vitamini C ina kazi muhimu katika mchakato wa kupona vidonda mwilini. Uhaba wake kwa muda mrefu unasababisha ugonjwa wa kiseyeseye (au hijabu). Kiseyeseye husababisha ufizi wa meno kuwa na vidonda na pia vidonda vingine mwilini kutopoa. Ugonjwa huu ulijulikana hasa wakati wa safari ndefu za baharini. Zamani haikujulikana chanzo chake kilikuwa nini; meli na jahazi zilibeba tu unga wa mkate au mchele kama chakula kilichoongezwa kwa nyama kavu au samaki kutoka baharini lakini matunda hayakuwa kawaida. Mabaharia wengi waligonjeka na kufa. Katika karne ya 19 mabaharia walitambua ya kwamba akiba ndogo ya malimau inaweza kuokoa watu kama wanakunjwa kijiko cha maji ya limau kila baada ya siku kadhaa.

Mwaka 1928 vitamini C iligundiuliwa pia kikemia na tangu 1928 ilithibitishwa kuwa inasmimamisha kiseyeseye.

Mahitaji ya mwili hukadiriwa kuwa miligramu 60-100 kwa siku; kiwango hiki kinapatikana kwa njia ya chakula cha kawaida.

Remove ads

Vyanzo

Matunda kama limau, chungwa na balungi ni vyanzo bora vya vitamini C. Kwa jumla karibu matunda yote yenye ladha ya kichungu ni chanzo chake.

Kuna pia aina za nyama na samaki zinazopeleka vitamini C mwilini. Hapo ndipo sababu ya kwamba Waeskimo hawakuwa na kiseyeseye ingawa zamani waliishi bila matunda kwa miezi mingi lakini walikula samaki bichi.

Kupika chakula kwa muda mrefu kunaharibu asidi ya vitamini C.


Maelezo zaidi Matunda, mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda ...
Maelezo zaidi Aina ya nyama, mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula ...


Remove ads

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads