Wakia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wakia (kutokana na Kiarabu: وقية - اوقية, awqiyah - waqiyah) unaweza kuhusu maana mbili:
Wakia wa kisasa
Wakia wa kisasa pia huitwa aunsi. Hufafanuliwa kuwa gramu 28.349523125, au 1/16 ya ratili.
Wakia asilia
Wakia asilia ni kipimo asilia kimojawapo cha Kiswahili ukitaja tungamo ya takribani gramu 28. Unafanana na kipimo cha Kiingereza cha aunsi (Kiingereza: "ounce"). Wakia wa dhahabu wa Kiingereza hufafanuliwa siku hizi kuwa gramu 31.1034768.
Waswahili wa zamani walipokea kipimo hiki kutoka lugha ya Kiarabu. Katika nchi za Kiislamu wakia ilikuwa sehemu ya 12 ya "ratl" (ratili) lakini ilhali jina la "ratili" iliweza kutaja uzani tofauti sana kati ya gramu 340 hadi kilogramu mbiloi, hata wakia zilitofautiana.[1] Wakia iliyotumiwa katika Afrika ya Mashariki ilifanana na wakia. Matumizi yake ilisanifishwa kwa kutumia sarafu ya reale kama uzani sanifu.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads