Kabila la Lawi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kabila la Lawi (kwa Kiingereza Levi) ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli. Kabila hilo hutazamwa kama uzao wa Lawi. Musa alizaliwa katika kabila hilo.[1]
Ndilo kabila pekee lililoteuliwa na Musa kwa kazi ya ukuhani[2]. Kufuatana na taarifa katika Kitabu cha Kutoka, Musa alifanya azimio hilo baada ya kuona juhudi ya kabila lake wakati wa kuwaondoa wafuasi wa ndama ya dhahabu[3].
Wakati wa kuingia katika nchi ya ahadi, Walawi hawakupewa na Yoshua eneo maalum bali walipewa haki ya kupokea sehemu za sadaka na zaka.
Makuhani wa Israeli walikuwa sehemu ya kabila la Lawi. Hadi leo jina la Lawi kwa umbo la Kizungu "Levi" linapatikana kati ya Wayahudi.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads