Wilaya ya Mbinga Vijijini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilaya ya Mbinga Vijijini
Remove ads

Wilaya ya Mbinga ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Ruvuma yenye postikodi namba 57400.

Thumb
Mahali pa Mbinga (kijani) katika mkoa wa Ruvuma.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 353,683 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 285,582 [2] baada ya maeneo yake kadhaa kutengwa kuwa wilaya ya Nyasa mwaka 2012 na mji wa Mbinga kuwa halmashauri ya pekee mwaka 2015.

Wilaya hii imepakana na mkoa wa Iringa upande wa kaskazini, wilaya za Songea mjini na Songea vijijini upande wa mashariki, Msumbiji upande wa kusini na Ziwa Nyassa upande wa magharibi.

Sehemu kubwa ya eneo lake iko ndani ya milima inayoongozana na pwani ya ziwa pamoja na mwambao wa ziwa.

Wilaya imeona maendeleo kadhaa kutokana na barabara mpya na kilimo cha kahawa inayostawi vizuri katika hali ya hewa mlimani.

Mji wa Mbinga ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Mbinga.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads