Mkoa wa Ruvuma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Pia unapakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Njombe na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki. Eneo lote ni la km2 63,669. Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794 (sensa ya mwaka 2022). Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.
Remove ads
Wilaya
Ndani ya mkoa huo kuna wilaya nane ambazo ni (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022[1]):
- Nyasa (191,193)
- Songea Mjini (286,285),
- Songea Vijijini (178,201),
- Tunduru (412,054),
- Madaba (65,215),
- Mbinga Vijijini (285,582),
- Mbinga Mjini (158,896),
- Namtumbo (271,368).
Wakazi
Makabila makubwa huko Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri kubwa ya Peramiho ya watawa Wabenedikto na nyingine iko Hanga.
Elimu
Elimu bado inahitajika, hasa kwa maeneo ya vijijini, maana watu wengi katika mkoa huu hawajaelimika hivyo huleta changamoto katika maendeleo maana taifa huhitaji watu ambao ni wasomi.
Miundombinu
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ni kiwango cha lami kuanzia Songea mjini kupitia Wilaya za Namtumbo, Tunduru, Nanyumbu, Masasi, Mnazimmoja-Lindi, hadi Dar es Salaam.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Songea Mjini : mbunge ni Leonidas Tutubert Gama (CCM)
- Nyasa : mbunge ni Stella Manyanya (CCM)
- Tunduru Kaskazini : mbunge ni Ramo Matala Makani (CCM)
- Tunduru Kusini : mbunge ni Daimu Iddi Mpakate (CCM)
- Peramiho : mbunge ni Jenista Mhagama (CCM)
- Madaba : mbunge ni Joseph Kisito Mhagama (CCM)
- Namtumbo : mbunge ni Edwin Amandus Ngonyani (CCM)
- Mbinga Mjini : mbunge ni Sixtus Mapunda (CCM)
- Mbinga Vijijini : mbunge ni Martin Msuha (CCM)
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads