Wimbo Ulio Bora
wa ishirini kitambo kitabu Biblia, mchanganyiko 8 sura ya, kama aongea juu ya ya historia Solomoni, kama lishangilia ya vifua na ya fupi-tumbo malka Sheba From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Utunzi wake
Ingawa mapokeo yanamtaja mfalme Solomoni kama mtunzi, wataalamu wanaona ni kazi ya mwandishi wa karne ya 4 KK aliyekusanya nyimbo mbalimbali za mapenzi.
Aina ya uandishi
Ni kati ya vitabu vya kishairi na vya pekee zaidi katika Biblia, kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili, ambao wanatafsiriwa kama wawakilishi wa Mwenyezi Mungu na taifa lake, kadiri ya moja kati ya mafundisho makuu ya ufunuo, linalotokana na nabii Hosea.
Ndio ujumbe wa kitabu: upendo kati ya mume na mke unaweza na kutakiwa kufanana na ule kati ya Yesu Kristo na Kanisa lake.
Maneno ya bibiarusi (Wim 8:6-7)
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads