Witness Mwaijaga Sigbjorn

From Wikipedia, the free encyclopedia

Witness Mwaijaga Sigbjorn
Remove ads

Witness Mwaijaga Sigbjorn (anafahamika kwa jina lake la kisanii kama Witness Kibonge Mwepec au kabla ya kuwa mshindi wa Coca Cola Pop Stars alifahamika kama Bad Gear; amezaliwa 15 Novemba 1982) ni msanii wa hip hop na rapa kutoka nchini Tanzania.

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Pia anajulikana kama ...
Remove ads
Thumb
Aliyekuwa msanii wa muziki nchini Tanzania

Anafahamika zaidi kwa kuwa mmoja kati ya washindi wa shindano la Coca Cola Pop Stars na mmoja wa wa wanzilishi wa kundi la muziki wa hip hop maarufu kama Wakilisha. Anavuma kwa baadhi ya vibao vyake kadhaa alivyofanya na kundi, pamoja na vya peke yake. Vibao hivyo ni pamoja na: Hoi, Kiswanglish, Kichekesho na [[Zero] n.k pia ana album yake inaitwa Khaya Khaya yenye nyimbo kumi, Iliyofanywa Tanzania na kuuzwa nchini Norway chini ya Lebo iitwayo Nedland Kultur.

Witness Kibonge Mwepec, alisoma katika Shule ya Msingi ya Oysterbay ya jijini Dar es Salaam, vilevile Shule ya Sekondari ya Jitegemee ambapo ndipo alipomalizia. Pia, alishafanya kazi na mashirika ya kimataifa kama vile UNICEF na alikuwa akifanya mikutano inayohusiana na masuala ya vijana.

Pia, alishawahi kuwa mcheza wa ngoma za asili na muziki wa asili yaani kuimba kwa kutumia ala za asili pia alikua ni muelimishaji rika wa ISHI, shirika la masuala ya mafunzo, uhamasishaji, uelimishaji rika na maendeleo ya vijana Tanzania.

Remove ads

Viungo vya nje

  • Witness katika Tanzania Directory.info
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Witness Mwaijaga Sigbjorn kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads